News
Kenya Police Bullets Mabingwa KWPL

Kilabu ya akina dada Kenya Police Bullets ndiyo mabingwa wa ligi ya taifa akina dada kwpl baada ya kuwanyuka Trinity starlets magoli 4-0 mechi ya mwisho hapo jana ugani afraha stadium Nakuru
Winga matata Emily Kemunto moranga alifungua ukurasa wa magoli dkaika 40,kisha Mshambulizi matata Rebecca Becky Okwaro akifunga magoli matatu dakika ya 55 ,dakika ya 79 na dakika 89 na kuchukua kiatu cha dhahabu kwa kufunga magoli 16 msimu huu
Kocha wa Bullets Beldine Odemba hakuficha furaha yake baada ya kushinda kombe hilo kwa mwaka wa pili mfululizo akitaja kwamba upinzani ulikua mkali ila wasichana wake wamepigana mpaka siku ya mwisho kubeba taji hilo.
Katika matokeo mengine
Kisped Queens 2-1 Vihiga Queens
Bunyore Starltes 0-3 Bungoma Queens
Kibera soccer Women 7-0 Mombasa olympic
Ulinzi Starlets 4-0 Kisumu All Starlets
JEDWALI
Bullets alama 46
Ulinzi starlets 45
Kibera soccer alama 42
Kayole starlets ni mabingwa wa KWNSL Baada ya kunyuka kayolets 3-0 madira soccer assasin
Iron ladies 3-0 Diani Quens na kushinda taji la fkf divisheni ya kwanza.
News
Rais Ruto Awaomba Radhi Watanzania.

Rais William Ruto amejitokeza na kuomba msamaha kwa niaba ya vijana wa Gen Z dhidi ya utawala wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Rais Ruto ameisihi serikali ya Tanzania kuondoa hofu kuhusu Mabishano makali ya Mtandaoni baina ya mataifa haya mawili licha ya Viongozi wa mataifa haya mawili Rais William Ruto na Mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuonekana kujaribu kuuzima moto wa mashambulio ya mitandaoni hasa miongoni mwa vijana wa Gen Z.
Akizungumza wakati wa dhifa ya asubuhi ya maombi ya kitaifa yaliondaliwa jijini Nairobi, Rais Ruto amesema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano mwema wa kidiplomasia na wala sio kuchangia uhasama, akiwaomba msamaha pia vijana wakenya.
Viongozi wahudhuria dhifa ya asubuhi ya maombi ya kitaifa
Kauli ya Rais Ruto imejiri baada Bunge la Tanzania kulazimika kusitisha vikao vya kawaida na kujadili hoja inayotajwa kugusia usalama wa taifa la Tanzania huku wakimpongeza rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyochukua ya kuwafurusha Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wakiongozwa na Martha Karua ambaye kiongozi wa chama cha People’s Liberation Party nchini Kenya na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga, Mwanaharakati Boniface Mwangi wa Kenya na Agather Atuhaire wa Uganda.
Mwanaharakati Bonifance Mwangi alipatikana katika eneo la mpakani mwaka Kenya na Tanzania katika eneo la Lunga lunga ilihali mwenzake Agather Atuhaire akipatikana karibu na kituo cha mpakani na Mtukula.
News
Manusua wa Mkasa Baharini, Kilifi

Mafisa wa uokoaji kaunti ya Kilifi bado wanaendelea kupiga mbizi baharini kutafuta Mwili wa Mwanabaharia mmoja Kapteni Kivondi, aliyezama Jumamosi usiki wa tarehe 24 Aprili, akiwa na wengine wawili katika mkono wa Bahari mjini Kilifi.
Kapteni Kivondi alifariki pamoja na mwenzake Kapteni Mwidini wakati wa mkasa huo, huku baharia mwengine wa tatu Aisha Jumwa akinusurika baada ya kuogelea baharini kwa zaidi ya masaa 16.
Akizungumza na CocoFm iliyomtembelea Hospitalini mjini Kilifi, Jumwa alielezea matukio hayo wakati mawimbi makali yalipopiga chombo chao na kukizamisha.
Mwili wa baharia mwengine ambaye alikuwa msaidizi wa nahodha wa Dau hilo, Kapteni Mwidini ulipatikana katika ufuo wa Watamu, umbali wa kilomita 50 kutoka mji wa Kilifi. Mwili wa marehemu uliondolewa na kusafirishwa hadi eneo la Likoni Mjini Mombasa kwa Maziko.
Aisha Jumwa -Manusuru wa mkasa wa baharini mjini Kilifi
Jumwa anasema kuwa aliweza kuokolewa siku iliyofuatia ya Jumapili, mwendo was saa sita adhuhuri baada ya kuogelea kwa maasaa hayo 16 licha ya upepo na mawimbi makali yaliyozidi kumsukuma maji makuu.
Kisa hiki kilitokea masaa machache tu hata baada ya idara ya Utabiri wa hali ya hewa kutoa tahadhari ya kuchafuka kwa Bahari na marufuku ya kuepuka fuo za bahari.
Hata hivyo Jumwa anasema kuwa tahadhari hiyo iliwapata kuchelewa hadi mkasa huo ulipowakuta. Anaongeza kwamba baada ya Dau lao kuzama watatu hao walijifunga Kamba ili waweza kuolea na kusaidiana lakini wawili hao wakashindwa na nguvu ya mawimbi hayo makali na kuaga dunia mikononi mwake
Taarifa ya Lolani Kalu