Connect with us

News

Wanaharakati wa Kutetea Haki za Kibinadamu Waandamana Mombasa

Published

on

Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu kaunti ya Mombasa wamefanya maandamano hadi katika ofisi za ubalozi wa Tanzania mjini Mombasa wakitaka kuachiliwa huru kwa Mwanaharakati wanaozuliwa nchini Tanzania.

Wakiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Haki Afrika Wakili Yusuf Abubakar, Wanaharakati hao wamesisitiza umuhimu wa haki za kibinadamu kulindwa huku wakiitaka serikali ya Tanzania kuheshimu haki za Wanaharakati hao.

Wakili Abubakar amesisitiza kuachiliwa kwa Wanaharakati hao huku akilaani vikali kuzuiliwa kwao, akisema Wanaharakati hao walizuru taifa hilo kufuatilia kesi ya Kiongozi wa upinzani nchini humo Tundu Lisu.

Kwa upande wake Afisa wa masuala ya dharura katika Shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI Francis Auma ametaka Wanaharakati Boniface Mwangi na Agather Haire ambao bado wanazuliwa nchini humo waachiliwe mara moja.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Watu watatu wakamatwa katika Mahakama ya Milimani

Published

on

By

Watu watatu wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa kaunti ya Trans Nzoia wamekamatwa na maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia sare baada ya kusikiza kesi inayomkabili gavana wa kaunti hiyo George Natembeya katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi.

Watatu hao walikamtwa mda mfupi baada ya Jaji Zipporah Gichana, kuagiza upande wa mashtaka kuwasilisha ushahidi dhidi ya kesi ya ufisadi inayomkabili gavana huyo.

Agizo hilo lilifuata tamko la upande wa mashtaka kwamba ilifeli kufuta agizo la awali la Mahakama la kuwasilisha ushahidi.

“Nyaraka na taarifa hizo zilipaswa kuwa zimetolewa kufikia sasa, kwa hiyo ninaelekeza upande wa mashtaka kufuata maagizo ya awali”, aliagiza Jaji Gichana.

Upande wa mashtaka uliomba mda wa wiki mbili zaidi ili kutii maagizo ya awali ya kuwasilisha ushahidi wa nyaraka.

“Hati nyingi zinapatikana kutoka kaunti ya Trans Nzoia na tumeshindwa kuzipata, tunaomba wiki mbili za ziada ili kutii,” Wakili wa Serikali Victor Awiti aliwasilisha.

Hata hivyo, upande wa utetezi ulipinga ombi hilo, ukisema ni sawa na matumizi mabaya ya mchakato wa Mahakama.

Upande wa mashtaka uliamriwa kufichua nyenzo zote husika kabla ya Juni 16 kesi hiyo itakapotajwa.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

News

Bitok: Wanafunzi wa Gredi ya 9 kutumia KEMIS kujiunga na shule za Upili

Published

on

By

Wanafunzi wa Gredi ya 9 watajiunga na shule za sekondari mwaka ujao kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa kuwasajili wanafunzi maarufu kama KEMIS.

Kulingana na Katibu katika Wizara ya Elimu nchini Julius Bitok, Serikali imebuni mfumo huo wa kieletroniki ili kuhakikisha wanafunzi wote walioko Gredi ya 9 wanajiunga na shule za sekondari.

Bitok ametangaza kwamba wanafunzi milioni 1.2 walioko Gredi ya 9 watajiunga na Gredi ya 10 katika shule za sekondari mwakani.

Mfumo huo wa kieletroniki uliovumbuliwa wiki iliyopita jijini Nairobi utanakili wanafunzi wote nchini kuanzia shule za Chekechea, msingi, upili, taasisi za kiufundi na vyuo vikuu.

Awali Wizara hiyo ilikuwa ikitumia mfumo wa NEMIS kuchukua takwimu za wanafunzi katika shule za umma ili itume mgao wa fedha za elimu ya bure kisha baadaye ikabadili hadi KEMIS huku kamati ya bunge kuhusu elimu ikiongozwa na Mwenyekiti wake Julius Melly ikiunga mkono mfumo huo na kuitaka Wizara hiyo kuhakikisha inanakili wanafunzi wote nchini.

Bitok amesema kila mtoto atapata nafasi katika shule za sekondari licha ya kuwa na shule chache za sekondari nchini.

Kulingana na takwimu katika Wizara hiyo kuna shule elfu 10 za sekondari huku idadi ya wanafunzi ikiwa kubwa mno ikilinganishwa na shule za sekondari.

Taarifa ya Elizebeth Mwende

Continue Reading

Trending