Sports
Kombe La Dunia Kwa Vilabu Kuingia Robo Fainali

Mashindano ya kombe la dunia baina ya vilabu kuingia katika hatua ya robo fainali hii leo nchini Marekani.
Al-Hilal iliobanduwa Manchester city chini ya Kocha Simeoni Inzaghi kushuka dimbani usiku wa leo ugani Camping Stadium kule Orlando saa nne usiku.
Kesho Asubuhi saa kumi ni zamu ya Chelsea dhidi ya Palmeiras ya Brazil ,Mabingwa Ligi ya Mabingwa UEFA PSG watakua uwanjani Saa moja usiku kuvaana na Bayern Munich ya Ujerumani.
Kisha saa stano usiku ni zamu ya miamba wa Uhispania Real Madrid kumenyana na wakilishi wengine wa Ujerumani Borrusia Dortmund.
Sports
Harambee Stars Kundi La Kifo Kundi B.

Sports
Kiungo Wa Brenford Bryan Mbeumo Sasa Ni Mali Ya United

Baada ya vute ni kuvute ambayo imedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ni rasmi kwamba kilabu ya manchester United na Brenford wameafikia makubaliano ya pauni milioni 70 ya kiungo mshambulizi Bryan Mbeumo raia wa Cameroon.
Haya yanajiri baada ya ofa mara mbili ya united kukataliwa na kilabu hio kabila ya kutuma ofa ya mwisho ya pauni milioni 65 na nyongesa ya pauni milioni 5.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano baada kukubali matakwa yake binafsi.
Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha mkuu Ruben Amorim baada ya ujio wa mshmabulizi Matheus Cunha.