Sports
Cherotich Na Yavi Kuzindua Uhasama Tena,Oregon
Bingwa wa nishani ya fedha mbio za olimpiki mitaa 3000 kuruka maji na viunzi Faith Cherotich anatarajiwa tena kuzindua uhasama na bingwa wa Olimpiki raia wa Bahrain Winfried Yavi na Mganda Peruth Chemutai katika msururu wa Prefontaine Classic Diamond League kule Eugene, Oregon Marekani hapo kesho.
Raia huyo anaingia kwenye mbio hizo akiwa na mortisha ya hali ya juu baada ya kushinda Yavi katika misururu mitatu msimu huu mbio za Doha nchini Qatar,Oslo kule Norway na Brussels.
Cherotich akiwa tayari amekusanya alama 24 dhidi ya 14 ya Yavi kuelekea katika msururu mwingine mjini Monaco Ufaransa Julai 11.
Msimamo wa 2025 Wanda Diamond League – Women’s 3000m hadi sasa;
Faith Cherotich (KEN) – 24 pts
Winfred Yavi (BRN) – 14 pts
Sembo Almayew (ETH) – 12 pts
Maraw Bouzayani (TUN) – 10 pts
Peruth Chemutai (UGA) – 9 pts
Lea Meyer (GER) – 8 pts
Courtney Wayment (USA) – 7 pts
Gabrielle Jennings (USA) – 6 pts
Norah Jeruto (KAZ) – 5 pts
Lomi Muleta (ETH) – 4 pts